
Dopa smartphones ni wafanyabiashara wanaojihusisha na biashara za simu za aina zote iPhone, Samsung, Oppo, Infinix, Tecno, Nokia, Redme, Itel na nyingine nyingi. Tuna matawi mengi Dar es Salaam; Mlimani City, Sinza Mori, Makumbusho, Kariakoo yote ni kurahisisha huduma kwa wateja wetu.
Pamoja na kuwa na matawi yote hayo ila bado tunafanya free delivery popote pale Dar es salaam kwa maana kwamba mteja kwetu ni mfalme.
NAMNA YA KUNUNUA SIMU HAPA
Tunauza Simu mpya na used zenye hali nzuri yote ni kumpatia mteja machaguo mengi kutokana na mahitaji yake.
Warranty mwaka mmoja
Simu mpya zina warranty ya mwaka mzima kama ukipata shida ya simu yako na ipo ndani ya warranty usisite kututaarifu muda wowote na utasaidiwa kadri inavyofaa.
Unafika ofisini kununua simu ukiwa na Oda tayari… kwa kuweka Oda hapa (ambapo utaona chini ya simu imeandikwa “Nunua” –utaweza kubonyeza pale na kuchati moja kwa moja kwa whatsapp na mmiliki wa duka kwa kuweka makubaliano ya bei na wapi utachukulia simu yako).
Pia tunafanya delivery sehemu husika ndani ya Dar na mkoani kwa haraka sana kwa wale watakaoshindwa kufika ofisini kutokana na ubusy wa maisha na unapewa risiti na warranty yako.
DELIVERY/USAFIRISHAJI
Mikoani na nchi jirani pia simu tunatuma na usafiri ni bure.
Tuna mawakala wetu kwa ajili ya usafirishaji wa simu mikoani na nchi jirani ambapo ikitokea ikapotea njiani kabla haijakufikia tutawajibika, ila pia una nafasi ya kuchagua kampuni ya usafirishaji unaotaka nje ya sisi na tutaufikisha sehemu hiyo na risiti tutakutumia na hapo itakuwa ni jukumu lako kuwasiliana nao na kama utapotea njiani hatutahusika kwa namna yeyote ile.
UNAWEZA UZA SIMU YAKO HAPA
Pia tunampa nafasi mtanzania kuweza kuuza simu yake kwenye hii website ukiwa popote pale Tanzania ukiwasiliana nasi kwa kusaidiana na mawakala wetu
UTARATIBU WA KUUZA SIMU YAKO NA MNUNUAJI:
Muuzaji atatupa taarifa na uzima wa simu yake na kama ina shida yeyote utasema na kama charger na Earphone zipo..na mkoa uliopo na ni sehemu gani.
- Kwa wale ambao wataweza kufika ofisini kwetu na simu ikaonwa na mafundi wetu na tukathibitisha taarifa alizotoa kuhusu simu kwamba ni sahihi basi kwenye tangazo la hiyo simu tutaandika -imekaguliwa–.
Ushauri kwa muuzaji wa simu: - Tunashauri muuzaji wa simu, kuifanyia simu marekebisho kama ina matatizo kabla ya kuchukua jukumu la kuiuza ili kuiongezea thamani na Ubora na pia ili iwe yenye manufaa kwa mnunuaji.
- Unaweza fika ofisini kwetu tuna mafundi wazuri na tukairekebisha kwa gharama nafuu.
Namna Biashara Inavyofanyika: - Kutakuwa na fomu za makubaliano wakati wa kufanya biashara kama mnunuaji atataka kuwa na uhakika wa alichokinunua na usalama(yaani sio cha wizi) kutoka kwa aliyemuuzia na shahidi atakuwa wakala wetu,popote pale Tanzania.
- Wakala wetu ndo atachagua sehemu ya kukutana ambayo ni salama na itakuwa ni karibu kwa kila mtu kwa kuzingatia makubaliano.
- Watanzania sisi ni waungwana tukiamini maisha bado yanaendelea kuna leo na kesho,tunafanya biashara kwa kuaminiana bila maandishi, ila kama mnunuaji atahitaji maandishi basi muuzaji na mnunuzi itabidi kila mmoja awe na passport size zisizopungua tatu,ambapo muuzaji,mnunuaji na wakala wetu kila mmoja atabakia na nakala(copy) moja yenye picha ya muuzaji,mnunuaji na wakala wetu kama ushahidi.
UFUNDI
Tuna huduma ya ufundi na mafundi wetu ni wa uhakika na wabobezi shida yeyote ukipata wasiliana nasi.
UZOEFU
Tumefanya biashara za simu kwa Muda sasa na watu mbalimbali na wamekubali uzoefu wetu,(wafanyabiashara ,wafanyakazi, wasomi mbalimbali kama madaktari,mainginia wahasibu walimu na wengine wengi) Baadhi yao utaweza kuwaona ukishuka chini ya page ya kwanza(yaani home page) na namna wanavyokubali huduma yetu.
(MUHIMU SANA)
Wasiliana na mmiliki moja kwa moja wa Dopa Smartphones kabla na baada ya kufanya biashara au huduma yeyote maana ndo kinga yako shida yeyote Ukiipata atawajibika.
Whatsapp/piga 0654484636.
Uaminifu, Ubora, Usalama ndio misingi yetu.
KARIBUNI SANA